Exodus 27:9-14

9 a“Tengeneza ua kwa ajili ya Hema la Kukutania. Upande wa kusini utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja,
Dhiraa 100 ni sawa na mita 45.
na utakuwa na mapazia ya kitani iliyosokotwa vizuri,
10pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo. 11Upande wa kaskazini utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja, nao utakuwa na mapazia, pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, pamoja na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo.

12“Upande wa magharibi wa ua utakuwa na upana wa dhiraa hamsini,
Dhiraa 50 ni sawa na mita 22.5.
nao utakuwa na mapazia, na nguzo kumi na vitako vyake kumi.
13Upande wa mwisho wa mashariki jua linakochomoza, ua pia utakuwa na upana wa dhiraa hamsini. 14Mapazia yenye urefu wa dhiraa kumi na tano yatakuwa upande mmoja wa ingilio, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu.
Copyright information for SwhKC